Monday, September 24, 2018

Mwanamuziki mbishi Willy Paul awashauri wanaume dhidi ya kuoa wanawake warembo.by jeff awala

  • Willy Paul alidai kuoa wanawake warembo ni kama kukaribisha shinikizo maishani .Mashabiki wake walifurahia sana kauli yake na kumsifu Mwanamuziki mbishi Willy Paul kwa mara ya kwanza ameungwa mkono na mashabiki wake na Wakenya kwa ujumla baada ya kutoa ushauri kwa wanaume. Nyota huyo amekuwa akikosolewa mara kwa mara na mashabiki wake kwa kila hatua, ikiwemo ni pamoja na nyimbo anazotoa. 
  • Hata hivyo, Ijumaa, Septemba 21, katika akaunti yake ya Instagram alishauri wanaume dhidi ya kuoa wanawake warembo. Kulingana na nyota huyo, kuoa mwanamke mrembo ni kujiletea ‘stress’ badala ya furaha. Pozee, kama anavyojulikana na mashabiki wengi alidai kuwa watu na mashabiki wanaweza kukusifu kwa kuoa mwanamke mrembo lakini hawawezi kuelewa unachopitia kwa kumuoa. Kulingana naye, mwanamke mrembo huja na changamoto zake, ikiwemo ni pamoja na ‘kukatiwa’ na wanaume wengi kwa sababu ya urembo wake. 
  • ''Ukioa mwanamke mrembo utasifiwa na marafiki, lakini utalia kila usiku nyumbani mwako,” aliandika katika akaunti yake ya Instagram. Kauli yake ilishangiliwa na maelfu ya mashabili ambao walimsifu kwa kuongea kitu kinachoweza kueleweka. Lakini wengi hawakushangaa kwa sababu siku hizi, nyota huyo amekuwa akishauri Wakristo vizuri. 
    jeffawala@gmail.com
  • jeffawalamusic.blogspot.com

1 comment:

Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa jeffawalamusic.blogspot.com nichapishe? Wasiliana nami kwa jeffawalamusic.blogspot.com, jeffawala@gmail.com , kwenye nambari: 0723410366 na kwenye facebook: jeff platnezz..

Do you have a hot story or scandal you would like me to publish, please reach me through jeffawala@gmail.com or telephone: 0723410366 and facebook: jeff platnezz jeffawalamusic.blogspot.com