Friday, August 24, 2018

Mbosso- Ujana Ulinipelekea Kupata Watoto Katika Umri Mdogo.

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Maromboso au maarufu kama Mbosso amekiri kuwa na watoto wawili katika umri mdogo ni matokeo ya balehe.
Mbosso ambaye kwa hivi sasa anaendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya “Nadekezwa” ni Baba wa watoto wawili ambao watoto wote wana umri sawa lakini ni mama tofauti.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Mbosso amekiri kuwa pamoja na kila mmoja kuwa na mama yake lakini hana uhusiano na kama zao kwa sasa kila mmoja ameshaolewa.
"Sipendi kuwa muongo na sitakuwa na dhambi ya uongo, huwa inatokea katika ukuaji (balehe) hususani sisi watoto wa kiume, kuna vitu utajizuia navyo lakini hutashindwa tu.
Kwa hiyo sitaki kuwa muongo, ilitokea ikawa hivyo nimekuwa baba nina watoto wangu wawili, tunaishi vizuri“.
Mbosso alianza muziki katika umri mdogo baada ya kujiunga Kwenye kundi la muziki la Yamoto Band miaka kadhaa.

No comments:

Post a Comment

Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa jeffawalamusic.blogspot.com nichapishe? Wasiliana nami kwa jeffawalamusic.blogspot.com, jeffawala@gmail.com , kwenye nambari: 0723410366 na kwenye facebook: jeff platnezz..

Do you have a hot story or scandal you would like me to publish, please reach me through jeffawala@gmail.com or telephone: 0723410366 and facebook: jeff platnezz jeffawalamusic.blogspot.com