Tuesday, November 13, 2018

Diamond Platinumz autetea wimbo wake chafu uliopigwa marufuku, adai ni ya watu wazima .By Jeff Awala.


  • Msanii maarufa Afrika Mashariki Diamond Platinumz amejitokeza na kukitetea vikali kibao chake ‘Mwanza’ kwa chapisho ndefu mtandaoni .KWA WAZEE WANGU WA BARAZA LA SANAA TANZANIA (BASATA) 
    Kwanza kabisa niwapongeze kwa kazi nzito na nzuri Mnayoifanya....lakini pia niwape pole kwa changamoto mbalimbali mnazokutana nazo, maana najua ugumu mnaopitia katika kusimamia sanaa yetu Nchini.....Ujumbe wenu kuhusu Kufungiwa wimbo wa #Mwanza almaarufu kama #NYEGEZI wakuu nimeupata ila tu kwabahati mbaya mtoto wenu niko Canada katika harakati za kutafta rizki ili kuendelea kulijenga taifa na kuendelea kutangaza sanaa zetu, ila laiti ningelikuwa nchini ningekujamara moja kama mnavyonijuaga pindi mniitapo basi hufika haraka bila ukaidi.....
    Tuki wama Wasani ambao tumesajiliwa tuna kila haki ya kuheshimu na kutii baraza letu la sanaa BASATA pindi linapotoa tamko.....kwasababu wao ndio wazazi na walezi wetu kwenye hii sanaa....na kwakutambua kuwa Sanaa ni kazi ya Ubunifu, na kwenye kubuni wakati mwingine kuna kuwa na usawa na wakati mwingine kutokuwa sawa ndiomaana mliteuliwa Nyinyi wazee wetu maalum kwa jili ya kuhakikisha wasanii wanapotoka nje ya Mstari mnawarudisha ili tuwe na sanaa ilio bora, tuzidi kufanikiwa, na kukua vyema na hata wasanii, mashabiki pamoja na taifa kwa ujumla lijivunie na linufaike na sanaa.....
    ila Kwenye UFUNGIWAJI huu nami nilikuwa nina OMBI ama PENDEKEZO kwa balaza letu pendwa la sanaa Tanzania (BASATA)....
    Licha ya kuwa ni kweli #NYEGEZI ni eneo na kituo cha Mabasi kilichopo MWANZA, lakini pia ni vyema Kama balaza letu pendwa la sanaa kutambua pia kuwa sio kila Nyimbo ni kwajili ya watoto wadogo....Hivyo kusema isipigwe kwenye TV na Radio tumekubali, lakini iwe Kwenye Ule muda ambao serikali uliuweka wa kuwa watoto wako macho, ila pale wanapolala, basi uruhusiwe ili walengwa wautazame.... PILI:- kusema tuifute Mitandaoni pia, naomba pia Baraza letu pendwa litutazame pia na hapo.... kwasababu mtoto mdogo tunaemlenga kumlinda asiharibikiwe kimaadili hapa, sizani kama mzazi wake anaweza kumruhusu akaperuziperuzi bila mipaka mitandaoni maana kama kweli ana uwezo wa kufanya hivyo basi anauwezo wa kwenda kuangalia hata Video za utupu, na vitu vingine ambayo wote tunafahamu ndio hatari na Madhara zaidi kwa watoto, kuliko hichi kinyimbo chetu cha #MWANZANYEGEZI.
  • Kulingana na msanii huyo, kibao chake hicho kiliwalenga watu wazima na wala si watoto na hivyo basi kudai kuwa hakuna haja ya kupigwa marufuku kibao hicho. Kupitia kwa chapisho lake ndefu, Diamond aliisihi bodi ya kusimamia usanii nchini Tanzania (Basata) kuondoa marafuku hiyo na kuiruhusu wimbo huo kuchezwa nyakati za usiku wakati watoto wote wamelala. Aliitaka serikli ya Tanzania kumpa uhuru wa utunzi maana ameipa umaarufu Tanzania kote duniani.a kumruhusu mtoto kutumia mitandao ya kijamaii bila idhini yao. Diamond alijiteteta zaidi akieleza kuwa kauli kama vile Nyegezi na Mwanza zilitotumika katika kibao hicho ni baadhi ya maeneo nchini Tanzania na wala si maneno machafu. Aliitaka serikali ya Tanzania kumpa uhuru wa utunzi maana ameipa umaarufu Tanzania kote duniani. 


Do you have a story you want told? Do you know of a sensitive story you would like me to get your hands on? Email your news TIPS to  jeffawala@gmail.com  Also contact me on 0723410366




No comments:

Post a Comment

Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa jeffawalamusic.blogspot.com nichapishe? Wasiliana nami kwa jeffawalamusic.blogspot.com, jeffawala@gmail.com , kwenye nambari: 0723410366 na kwenye facebook: jeff platnezz..

Do you have a hot story or scandal you would like me to publish, please reach me through jeffawala@gmail.com or telephone: 0723410366 and facebook: jeff platnezz jeffawalamusic.blogspot.com